3 Desemba 2025 - 13:44
Kikao cha Kamati ya Elimu cha Jamiat Al-Mustafa – Dar es Salaam, Tanzania +Picha

Kikao hiki kimeweka msingi muhimu kwa mustakabali wa elimu na malezi ndani ya Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam-Tanzania, huku wajumbe wakiahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu katika kuboresha mwelekeo wa kielimu na kijamii kwa manufaa ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kamati ya Elimu ya Jamiat Al-Mustafa (SA) tawi la Dar es Salaam imefanya kikao maalumu kujadili masuala muhimu yanayohusiana na maendeleo ya kielimu, kijamii na kiutamaduni ndani ya taasisi hiyo. Kikao hicho kililenga kupitia hali halisi ya mahitaji ya jamii na kuweka mikakati inayolenga kuinua ubora wa elimu na shughuli za malezi kwa mujibu wa misingi ya Kiislamu.

Kikao cha Kamati ya Elimu cha Jamiat Al-Mustafa – Dar es Salaam, Tanzania +Picha

Katika kikao hicho, wajumbe walijadili mada mbalimbali zenye uzito, ikiwemo:

  1. Mahitaji ya Kijamii na Mwelekeo wa Elimu:
    Wajumbe walitathmini namna mfumo wa elimu unavyochangia kutatua changamoto za kijamii, pamoja na kuweka mkazo juu ya kozi muhimu zinazohitajika katika mazingira ya sasa, hususan zinazohusiana na malezi, tabia na maendeleo ya mwanafunzi wa Kiislamu.

  2. Mfumo wa Malezi na Kuimarisha Mahusiano ya Wanajamii:
    Kikao kilijadili umuhimu wa kujenga jamii yenye mshikamano, maadili mema na uelewa wa pamoja juu ya misingi ya Kiislamu. Aidha, wajumbe walisisitiza umuhimu wa kufundisha mbinu za kimaingiliano (social relations) kulingana na maadili ya Qur’ani na Sunna.

  3. Utamaduni na Tabligh kupitia Mitandao ya Kijamii:
    Kwa kutambua ukuaji wa teknolojia, kikao kilitoa mapendekezo ya kuimarisha kazi za tabligh kupitia majukwaa ya kidijitali ili kufikisha ujumbe wa Kiislamu kwa umahiri, weledi na mtazamo chanya kwa jamii pana.

  4. Misingi ya Utafiti wa Kielimu na Uandishi wa Makala:
    Wajumbe walikubaliana juu ya kuimarisha uwezo wa wanafunzi na walimu katika sekta ya utafiti, ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kuandika makala zenye ubora wa kitaaluma zikilingana na viwango vya kimataifa.

  5. Ratiba na Mikakati ya Maendeleo ya Kitaaluma:
    Kikao pia kilipitia ratiba mbalimbali za masomo na programu za mafunzo, kwa lengo la kuhakikisha kuwa shughuli zote za kitaaluma ndani ya Jamiat Al-Mustafa zinakwenda sambamba na mahitaji ya sasa ya jamii na dira ya taasisi.

    Kikao cha Kamati ya Elimu cha Jamiat Al-Mustafa – Dar es Salaam, Tanzania +Picha

Kwa ujumla, Kikao hiki kimeweka msingi muhimu kwa mustakabali wa elimu na malezi ndani ya Jamiat Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam-Tanzania, huku wajumbe wakiahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu katika kuboresha mwelekeo wa kielimu na kijamii kwa manufaa ya wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Kikao cha Kamati ya Elimu cha Jamiat Al-Mustafa – Dar es Salaam, Tanzania +Picha

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha